Swali: Kuna mwanamke ambaye amefiliwa na mumewe na anaishi ar-Riyaadh na hana yeyote. Kaka yake anaishi Makkah. Je, inajuzu kwake kusafiri kwenda kwake na kufanya ´Umrah pamoja na Mahram wake?
Jibu: Hakuna neno ikiwa yuko khatarini, hawezi kubaki mwenyewe na hana yeyote ambaye anaweza kumliwaza. Lakini ikiwa yuko na wa kumliwaza, hayuko katika khatari, yuko na muhudumu wa kike, jamaa zake kama vile mamake mume na wengine wenye kumliwaza na kumwondoshea mawazo, haifai kwake kutoka mpaka pale itakapomalizika eda yake. Ama akiwa analazimika kufanya hivo hapana neno.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/6369/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B3%D9%81%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D8%AB%D9%86%D8%A7%D8%A1-%D9%81%D8%AA%D8%B1%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AF%D8%A7%D8%AF
- Imechapishwa: 27/12/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
168. Ni yepi yanayomlazimu mwanamke ambaye amefiwa na mume wake?
Swali 168: Dada anauliza ni yepi yanayomlazimu mwanamke ambaye amefiwa na mume wake[1]? Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth mambo ambayo anatakiwa kujiepusha nayo anayekaa eda. Kuna mambo matano yanayotakikana kwake: 1 – Kulazimiana na nyumba ambayo amekufa ndani yake mume wake ilihali anaishi ndani yake. Atatakiwa kubaki hapo mpaka pale itakapomalizika…
In "Ahkaam-ul-Janaa-iz - Ibn Baaz"
169. Ni vipi atakaa eda mwanamke mwajiriwa?
Swali 169: Mwanamke wa Kiislamu na ambaye ameajiriwa akifiwa na mumewe na anaishi katika nchi ambayo haimpi mtu yeyote aliyefiwa na ndugu yake likizo isiyozidi siku tatu. Ni vipi atakaa eda katika hali kama hii? Kwa sababu akiamua kukaa eda ule muda uliowekwa katika Shari´ah basi atafukuzwa kazini. Je, aache…
In "Ahkaam-ul-Janaa-iz - Ibn Baaz"
Kwanini mume yuko Marekani?
Swali: Kuna mtu anamzuia msichana wake kusafiri kwenda kwa mume wake anayeishi Amerika. Hoja yake ni kwamba watoto watakuja kukulia maisha ya kimagharibi katika mji wa kikafiri. Hata hivyo mume wake anataka aende. Je, inajuzu kwake kumkabidhi naye kwa kuzingatia ya kwamba atakuwa amemuasi baba yake? Jibu: Kwanza ni kwa…
In "Kuwatendea wema wazazi"