Swali: Kuna mtu anataka kulingania kwa Allaah na kufanya matendo mema lakini hata hivyo anaona kuwa harakati zake na mambo yake binafsi yanamchukua muda wake mwingi. Je, inafaa kwake kuchukua malipo juu ya matendo yake ikiwa nia yake ni njema?

Jibu: Ikiwa mtu anayo nia njema, basi Allaah humsahilishia kazi yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila kitendo kinategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.

Hili ni mosi.

Jengine ni kwamba mtu anatakiwa kupangilia wakati wake. Hakika nafsi yake ina haki, familia yake ina haki na mgeni wake ana haki juu yake. Kwa hivyo anapaswa kupangilia wakati wake ambao anaweza kuwatekelezea familia yake haki zao. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Swalah bora ya usiku ni swalah ya Daawuud; alikuwa akilala nusu ya usiku, akiswali theluthi yake na akilala sudusi yake.”[1]

Mtu akifanya kitendo hichi hali ya kumtakasia Allaah nia, basi Allaah atamsahilishia mambo hayo. Lakini kule yeye kutaka kuwa kiongozi katika elimu, kulingania na matendo mema pasi na kutikisika ni jambo lisilowezekana. Huyu anakumbushia yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Mwenye busara ni yule mwenye kuifanyia hesabu nafsi yake na akatenda kwa ajili ya yaliyoko baada ya mauti. Aliyeshindwa ni yule mwenye kufuata matamanio ya nafsi yake na huku akawa na matumaini batili juu ya Allaah.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).

[2] at-Tirmidhiy (2459) ambaye amesema ni nzuri, Ibn Maajah (4260), Ahmad (17123) na al-Haakim (1/57) ambaye ameisahihisha. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (263).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (19 B) Dakika: 29:47
  • Imechapishwa: 27/12/2020