Swali: Mwanamme kukaa chemba na wanawake wawili ni jambo limekatazwa?

Jibu: Hapana vibaya. Kukaa chemba kulikokatazwa ni mwanamke akiwa mmoja. Lakini wakiwa watatu pasi na fitina na pasi na tuhuma hapana neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamme asikae chemba na mwanamke. Kwani hakika shaytwaan ndiye watatu wao.”

Wakiwa kuanzia wawili na zaidi inaondoka chemba. Isipokuwa kukiwa kuna tuhuma.

Swali: Ijapo mwanamke atakuwa mtumzima?

Jibu: Hata akiwa mtumzima. Hadiyth ni yenye kuenea. Kila chenye kutupwa kina mwenye kukiokota.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22094/حكم-خلوة-الرجل-بالمراتين
  • Imechapishwa: 22/10/2022