Malipo ya mwenye kuapa hali ya kuwa ni mwongo

Swali: Baadhi ya watu wanasema:

“Mwenye kuapa kwa jina la Allaah hali ya kuwa ni mwongo Allaah atamkata mgongo wake.”

Je, huku ni kwa minajili ya kumtia khofu?

Jibu: Sijafikiwa na hilo. Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni:

“Yule mwenye kukata haki ya mtu muislamu basi Allaah amemuwajibishia Moto na amemuharamishia Pepo.”

Katika tamko lingine imekuja:

“Yule mwenye kuapa kiapo akiwa ni mwenye kumnyang´anya mali ya ndugu yake pasi na haki basi atakutana na Allaah hali ya kuwa amemkasirikia.”

Swali: Je, Allaah atamcheleweshea adhabu hiyo Aakhirah?

Jibu: Hiyo ni miongoni mwa adhabu zake. Pengine adhabu yake ikaharakishwa hapahapa duniani. Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22070/ما-جزاء-من-يحلف-كاذبا
  • Imechapishwa: 22/10/2022