Anayefanya matendo ya kishirikina kwa ujinga

Swali: Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah, anayazunguka makaburi na anafanya matendo ya kishirikina kwa ujinga.

Jibu: Afunzwe. Ni mshirikina kama washirikina kabla ya kuja Uislamu. Aamrishwe mpaka atubie.

Swali: Akifa juu ya hali hiyo anakufa akiwa ni mshirikina?

Jibu: Kama alikuwa akiyaabudu makaburi amekufa akiwa mshirikina. Hivyo hatoswaliwa, hatooshwa wala hatozikwa pamoja na waislamu.

Swali: Hata kama alikuwa mjinga?

Jibu: Hata kama alikuwa mjinga. Waabudia al-Badawiy na mfano wao ni katika makafiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22067/حكم-من-يعمل-امورا-شركية-جاهلا
  • Imechapishwa: 22/10/2022