Kulala baada ya ´Aswr na baada ya Maghrib

Swali: Je, kuna makatazo ya kulala baada ya swalah ya ´Aswr?

Jibu: Hakukupokelewa chochote. Sijui kama kumepokelewa chochote juu ya hilo. Isipokuwa baadhi ya maneno ya washairi. Lakini hayana mashiko. Hayazingatiwi.

Swali: Kwa hivyo hakuna ubaya?

Jibu: Hakuna neno. Hakuna ubaya.

Swali: Inachukiza kulala baada ya Maghrib?

Jibu: Ndio, inachukiza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22096/حكم-النوم-بعد-صلاتي-العصر-والمغرب
  • Imechapishwa: 22/10/2022