Kusema dawa fulani ndio imemponya mgonjwa

Swali: Msemo unaosema:

“Mgonjwa amejisikia vizuri kwa dawa hii.”

Jibu: Hapana, kusisemwi hivo. Matibabu haya ni sababu tu. Mtu anatakiwa kusema miongoni mwa sababu za Allaah kumponya ni kuwa amejitibu kwa dawa fulani, amefanya kitu fulani na amejikinga kwa kitu fulani. Hizi ni miongoni mwa sababu ambazo haitakiwi kunasibisha ponyo kwazo. Bali zinanasibishwa tu kuwa ni sababu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22097/حكم-قول-ما-طاب-المريض-الا-بهذا-العلاج
  • Imechapishwa: 22/10/2022