Mwanamke kujifunua mbele ya daktari wa kiume

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kujifunua mbele ya daktari wa kiume?

Jibu: Ni dharurah. Akihitaji kujifunua sehemu anayougua, basi atajifunua kwa kiasi kinachohitajika. Hili ni kutokana na dharurah. Haijuzu kwake kujitibu kwa daktari wa kiume akipatikana daktari wa kike. Aende kwa daktari huyu wa kike.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 10/04/2023