Mwanamke kuitikia simu na anayebisha mlango

Swali: Mmoja katika marafiki zangu akibisha mlango na mimi na nyumbani hakuna mtu zaidi ya mke wangu – anyamaze au aitikie salamu au aitikie na amweleze kuwa hayuko?

Jibu: Kukibishwa mlango ndani hakuna zaidi ya mke au simu ikaita hapana neno akaitikia salamu na hapana neno akaitikia mlango. Wanawake zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiitikia, wakizungumza na wakiwakaribisha wageni pamoja na usalama na kujitenga mbali na shari. Akiitikia na kusema hayupo. Akiuliza mahali alipo ni sawa akajibu kwamba yuko mahali fulani ikiwa kufanya hivo hakuna madhara yoyote. Katika hali hiyo hakuna ubaya.

Kilichokatazwa ni yale yanayopelekea katika fitina, faragha kati ya mwanaume na mwanamke au kulegeza sauti mpaka akatamaniwa. Amesema (Ta´ala):

فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ

”Msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi.” (33:32)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3685/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B1%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D9%87%D8%A7%D8%AA%D9%81-%D9%88%D9%85%D9%86-%D9%8A%D8%B7%D8%B1%D9%82-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D8%A7%D8%A8
  • Imechapishwa: 04/03/2020