Je, swawm inaharibika yakimrudi mtu matapishi kutoka kooni?

Swali: Nimepatwa na maradhi ya kupoza kwa figo katika mwezi wa Ramadhaan iliopita. Nimeweza kufunga na himdi zote anastahiki Allaah. Lakini baadhi ya masiku najiwa na matapishi ya nguvu kwa kiasi cha kwamba yanarudi kooni mwangu kwa mara nyingine. Je, katika hali hii swawm yangu inakuwa sahihi au hapana?

Jibu: Swawm ya muulizaji huyu ni sahihi. Kwa sababu matapishi haya ni pasi na kutaka kwake. Mmesikia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ambaye matapishi yatamshinda hana juu yake kulipa.”

Kikimrudi kitu kutoka kooni bila mtu mwenyewe kutaka hivyo hakuna juu yake kitu. Kwa sababu miongoni mwa sharti za kuharibika kwa swawm ni mtu awe amekusudia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1567
  • Imechapishwa: 04/03/2020