Mwanamke kuacha wazi miguu na viganja vya mikono

Swali: Ni ipi hukumu ya kuacha wazi miguu na viganja vya mikono kwa watu wa kando?

Jibu: Hukumu ni kwamba imekatazwa. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ

“Mnapowauliza [wake zake] haja yoyote, basi waulizeni nyuma ya pazia.”

Hili linahusu mwili wake mzima:

ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

“Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamke ni ´Awrah.”

Amesema tena (Jalla wa ´Alaa):

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ

“Na waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika; hivyo waangushe khimari zao mpaka vifuani mwao. Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, baba zao, baba za waume wao, wana wao wa kiume, wana wa kiume wa waume zao, kaka zao, wana wa kiume wa kaka zao, wana wa kiume wa dada zao, wanawake wao [dada zao wa Kiislamu], wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, watumishi wanaume wasio na matamanio [tena kwa wanawake], au watoto ambao [bado] hawaelewi [kitu kuhusu] yanayohusu uke. Na wala wasipige miguu yao [wanapotembea] yajulikane yale wanayoyaficha katika mapambo yao.”[2]

[1] 33:53

[2] 24:31

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4135/حكم-اظهار-الكفين-والقدمين-لغير-المحارم
  • Imechapishwa: 12/05/2020