Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

اتَّبِعُواْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلاَ تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاء قَلِيلاً مَّا تَذَكَّرُونَ

“Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu, na wala msifuate pasi Naye walinzi wengine.” – ni machache mnayoyakumbuka.”[1]

Yale yaliyoteremshwa kwenu ni Qur-aan na Sunanh vinavyoibainisha, na sio maoni ya wanamme. Amesema (Ta´ala):

وَذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودً

“Wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume”, basi utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.”[2]

Aayah hii tukufu imejulisha kwamba yule mwenye kuitwa kuitendea kazi Qur-aan na Sunnah lakini hata hivyo akavipa mgongo kwamba ni katika wanafiki. Kwa sababu kinachozingatiwa ni kuenea kwa matamshi na sio sababu maalum. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho.”[3]

Kurudi kwa Allaah na kwa Mtume Wake ni kurudi katika Kitabu Chake na katika Sunnah zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kufa kwake. Allaah ameifungamanisha imani na kitendo hicho pale aliposema:

إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“… mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho.”

Aayah inapata kufahamisha kwamba yule asiyerejea katika Qur-aan na Sunnah wakati wa mizozo sio muumini.

[1] 07:03

[2] 04:61

[3] 04:59

  • Mhusika: Imaam Muhammad al-Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Adhwaa’-ul-Bayaan (5/87)
  • Imechapishwa: 12/05/2020