Mwanamke anaomba talaka kwa mume ambaye wameishi naye zaidi ya miaka 30

Swali: Je, talaka ya mtu ambaye kwa sababu ya uzee hafanyi maamuzi vizuri huhesabiwa kuwa ni talaka? Mwanamke huyu ameishi naye zaidi ya miaka thelathini, hawajabarikiwa kupata mtoto na sasa anataka talaka. Je, ana dhambi au hana?

Jibu: Ikiwa amempa talaka hali ya kuwa anafahamu analolifanya, hajapoteza akili, wala hajachanganyikiwa na akili yake bado iko sawa, basi talaka hiyo huhesabiwa. Akitoa talaka hali ya kuwa akili yake iko pamoja naye, basi talaka imepita. Ama mwanamke ikiwa atasubiri na kuvumilia hali yake hilo ni bora zaidi, ni jema zaidi na bora zaidi. Lakini ikiwa atapata mashaka juu yake, kama vile mume kuwa mkali, kumuumiza au kuwepo sababu nyingine zinazoleta madhara, basi hakuna dhambi juu yake kuomba talaka. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke yeyote anayeomba talaka bila ya sababu… ”

Kuhusu mwanamke huyu amepata sababu na amepata madhara.

Kwa hiyo akipata madhara na kuumizwa, basi hapana kizuizi cha kumuomba talaka. Ikiwa atasubiri, akavumilia na akamtendea wema katika uzee wake, basi ana ujira mkubwa sana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2132/حكم-طلاق-من-لا-يحسن-التصرف
  • Imechapishwa: 19/07/2026