Mtoto anakiuka makubaliano ya ardhi

Swali: Imetufikia kutoka kwa mmoja wa ndugu muhtaswari wake ni huu: Nilimpa mwanangu mkubwa kipande cha ardhi ya ujenzi kwa sharti la mdomo kwamba manufaa yake yawe kwa familia yote na nikaandika hilo. Lakini yeye akajenga juu yake, akaitumia kwa manufaa yake binafsi na wala hakumpa yeyote kati yetu chochote na akakataa. Nilimtaka atekeleze Shari´ah ya Allaah, kwamba ainufaishe katika uhai wangu, kisha iwe ni urithi kila mmoja apate haki yake. Lakini akanitishia, akanitukana, akanivunjia heshima, akamtukana Allaah, akararua kitabu cha ”Minhaaj-ul-Muslim” na kukitupa. Je, nina dhambi juu ya yaliyotokea?

Jibu: Wajibu wako ni kuinua jambo lake mahakamani na uieleze mahakama kwa yaliyojiri. Mahakama kuna kheri ndani yake na baraka. Haya ni masuala ya mzozo kati yako na mwanao. Haya ni katika adhabu za upendeleo. Haya ni katika adhabu zako kwa kumtenga kwa kumpa kitu maalum peke yake. Mtoto hapaswi kubaguliwa kwa kumpa kitu bila wengine:

”Mcheni Allaah na fanyeni uadilifu kati ya watoto wenu.”

Ulipotokea upendeleo huu na kulegalega, ikawa haya ni katika aina ya adhabu.

Kwa hiyo wajibu juu yako ni kumkabili kwa mujibu wa Shari´a na kupeleka jambo lake kwa wenye mamlaka ili wakutoe katika uovu wa uasi wa mtoto, kukanusha haki na kuikataa na ili utekeleze uadilifu kati ya watoto wako.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2134/وجوب-المساواة-بين-الابناء-في-العطية-والهدية
  • Imechapishwa: 19/07/2026