Swali: Imesemwa katika ”Subul-us-Salaam”:

“Mwanaume akimfananisha mke wake na mama yake huku anakusudia talaka, basi itakuwa ni kumlinganisha na mama. Akimtaliki huku anakusudia kumlinganisha na mama yake, basi itakuwa ni talaka.”

Je, hili ni sahihi? Vipi kuoanisha hili na Hadiyth isemayo:

“Hakika matendo hutegemea nia.”?

Jibu: Allaah amefanya kumlinganisha mke na mama kuwa kama ilivyo, kwa sababu watu wa kipindi kabla ya kuja Uislamu walikuwa wanaifanya kuwa ni talaka. Basi Allaah akahukumu jambo hilo kuwa kama lilivyo na kwamba ni kuharamisha. Aidha akaweka wazi kafara yake katika Kitabu Chake kitukufu. Kwa hiyo haiwi talaka. Ikiwa atasema: “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu”, “kama mgongo wa dada yangu” au “kama mgongo wa binti yangu” basi huko ni kumlinganisha na mama yake hata kama amekusudia talaka. Bali ni kumfananisha mke na mama, kama Allaah alivyoweka katika Shari´ah, kinyume na matendo ya kipindi ya kuja Uislamu. Allaah amebatilisha matendo ya kipindi kabla ya kuja Uislamu. Kwa hiyo itakuwa na hukumu ya kumlinganisha mke na mama na juu yake kuna kafara; ni kuacha huru mtumwa, akishindwa, basi afunge miezi miwili mfululizo, akishindwa, basi awalishe chakula masikini sitini kabla ya kumjamii. Ama ikiwa atasema: “Wewe umeachika” huku anakusudia kumfananisha na mama yake, basi haiwi kumlinganisha na mama yake. Kwa sababu maneno haya hayaleti maana ya kumfananisha mke na mama. Maneno “Wewe umeachika” ni maneno ya wazi ya talaka, basi hayahamishwi kutoka kwenye maana ya wazi ya talaka kwenda kwenye maana nyingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2128/حكم-اعتبار-الظهار-طلاقا
  • Imechapishwa: 19/07/2026