Swali: Nakuarifuni kwamba mimi ni mfanyakazi na taasisi ninayofanyia kazi inakubali kuandikisha watu kazi ya muda nje ya kituo kwa vipindi mbalimbali, ilihali mtu aliyeandikishwa haendi kutekeleza kazi yoyote. Wakubwa wanajua hilo na wanaichukulia posho ya jambo hilo kuwa ni motisha kwa mfanyakazi, zawadi na kumtia moyo kwa kazi anayoifanya. Je, fedha ninazochukua kama posho ya jambo hilo ni halali au haramu?
Jibu: Kinachojulikana ni kwamba hili halijuzu, kwa kuwa anaandikwa kazi hali ya kuwa hakuandikishwa kweli, naye yuko kazini na hakuondoka. Kinachojulikana ni kwamba hili ni hila, ni uongo na ni udanganyifu kwa dola. Kwa hivyo ni haramu, kwa sababu hii ni dhuluma bila haki.
Ama ikiwa dola imefahamishwa jambo hili na ikawaridhia wakurugenzi kufanya hivyo kwa wafanyakazi wao na jambo hili likawa ni katika makubaliano ya dola na wasimamizi au mawaziri, basi hakuna tatizo. Kwa sababu dola huona maslahi. Ikiwa imeona kuwa inafaa kuwaandikisha baadhi ya watu kazi kivitendo na kuwapa posho kama zawadi ya kuwatia moyo kwa kazi yao – kama ambavyo hupewa aliye kazi ili kumsaidia katika kazi yake, huku asipate tabu ya safari, kuachana na familia na mfano wa hayo – ikiwa dola imeona hilo kwa lengo la kutuliza nyoyo za waliopo kazini, kuongeza bidii yao na kuwahimiza katika kazi, basi hilo ni juu ya dola. Lakini ikiwa ni mfanyakazi aliye juu yake anayeidanganya dola na kuighushi, kisha akampa kitu ambacho hakina uhalisia, basi kilicho dhahiri kwa misingi ya Shari´ah ni kwamba hili ni haramu na halijuzu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2143/حكم-اخذ-بدل-انتداب-دون-الذهاب-الى-ما-انتدب-اليه
- Imechapishwa: 19/07/2026
Swali: Nakuarifuni kwamba mimi ni mfanyakazi na taasisi ninayofanyia kazi inakubali kuandikisha watu kazi ya muda nje ya kituo kwa vipindi mbalimbali, ilihali mtu aliyeandikishwa haendi kutekeleza kazi yoyote. Wakubwa wanajua hilo na wanaichukulia posho ya jambo hilo kuwa ni motisha kwa mfanyakazi, zawadi na kumtia moyo kwa kazi anayoifanya. Je, fedha ninazochukua kama posho ya jambo hilo ni halali au haramu?
Jibu: Kinachojulikana ni kwamba hili halijuzu, kwa kuwa anaandikwa kazi hali ya kuwa hakuandikishwa kweli, naye yuko kazini na hakuondoka. Kinachojulikana ni kwamba hili ni hila, ni uongo na ni udanganyifu kwa dola. Kwa hivyo ni haramu, kwa sababu hii ni dhuluma bila haki.
Ama ikiwa dola imefahamishwa jambo hili na ikawaridhia wakurugenzi kufanya hivyo kwa wafanyakazi wao na jambo hili likawa ni katika makubaliano ya dola na wasimamizi au mawaziri, basi hakuna tatizo. Kwa sababu dola huona maslahi. Ikiwa imeona kuwa inafaa kuwaandikisha baadhi ya watu kazi kivitendo na kuwapa posho kama zawadi ya kuwatia moyo kwa kazi yao – kama ambavyo hupewa aliye kazi ili kumsaidia katika kazi yake, huku asipate tabu ya safari, kuachana na familia na mfano wa hayo – ikiwa dola imeona hilo kwa lengo la kutuliza nyoyo za waliopo kazini, kuongeza bidii yao na kuwahimiza katika kazi, basi hilo ni juu ya dola. Lakini ikiwa ni mfanyakazi aliye juu yake anayeidanganya dola na kuighushi, kisha akampa kitu ambacho hakina uhalisia, basi kilicho dhahiri kwa misingi ya Shari´ah ni kwamba hili ni haramu na halijuzu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2143/حكم-اخذ-بدل-انتداب-دون-الذهاب-الى-ما-انتدب-اليه
Imechapishwa: 19/07/2026
https://firqatunnajia.com/kuchukua-posho-ya-kazi-bila-kuwajibika/