Swali: Mimi niko katika mazingira ambamo maovu mengi yameenea na sijaona yeyote anayetekeleza kuamrisha mema na kukataza maovu, si kwa siri wala kwa wazi. Sijui kama nikisimama kuamrisha mema na kukataza maovu kunaweza kunipata madhara au madhara. Mimi nimeazimia kuamrisha mema na kukataza maovu, ni mamoja iwe ni misikitini au kwa watu mmoja mmoja. Ni njia zipi nichukue?
Jibu: Inakupasa kusimama kutekeleza hilo muda wa kuwa uko katika mazingira ambayo wajibu huo haufanywi na hujaona yeyote aliyeutekeleza. Basi tekeleza wajibu huo ikiwa una elimu na uelewa sahihi, kwamba jambo fulani limeachwa nalo ni wajibu kulitekeleza au kwamba jambo fulani limefanywa nalo ni ovu linalopaswa kukemewa. Ikiwa una uelewa sahihi, basi kemea maovu:
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ
“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi.”[1]
Kwa hiyo anza kwanza kujielimisha, ujifunze dini na uangalie dalili, kisha utekeleze wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, kulingania na kuwaelimisha watu kwa hekima, kwa maneno mazuri na kwa mwenendo mwema. Pia anza na nafsi yako kabla ya wengine ili uwe mfano mwema unaofuatwa katika kheri. Usikumbwe na uvivu wala udhaifu kama ilivyowapata wengi, bali vumilia, endelea kuwa na subira na muombe Mola wako msaada na tawfiyq. Aidha ni juu yako kutumia hekima, mtindo mzuri, subira na uvumilivu na kuchagua nyakati muafaka katika kuwakumbusha watu, kuwaalika kwenye kheri na kubainisha yale uliyoona katika jamii yako, nyumbani mwako, kabila lako au sehemu nyingineyo.
[1] 12:108
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2200/واجب-من-اقام-في-بيىة-فيها-منكرات-لم-تنكر
- Imechapishwa: 19/07/2026
Swali: Mimi niko katika mazingira ambamo maovu mengi yameenea na sijaona yeyote anayetekeleza kuamrisha mema na kukataza maovu, si kwa siri wala kwa wazi. Sijui kama nikisimama kuamrisha mema na kukataza maovu kunaweza kunipata madhara au madhara. Mimi nimeazimia kuamrisha mema na kukataza maovu, ni mamoja iwe ni misikitini au kwa watu mmoja mmoja. Ni njia zipi nichukue?
Jibu: Inakupasa kusimama kutekeleza hilo muda wa kuwa uko katika mazingira ambayo wajibu huo haufanywi na hujaona yeyote aliyeutekeleza. Basi tekeleza wajibu huo ikiwa una elimu na uelewa sahihi, kwamba jambo fulani limeachwa nalo ni wajibu kulitekeleza au kwamba jambo fulani limefanywa nalo ni ovu linalopaswa kukemewa. Ikiwa una uelewa sahihi, basi kemea maovu:
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ
“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi.”[1]
Kwa hiyo anza kwanza kujielimisha, ujifunze dini na uangalie dalili, kisha utekeleze wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, kulingania na kuwaelimisha watu kwa hekima, kwa maneno mazuri na kwa mwenendo mwema. Pia anza na nafsi yako kabla ya wengine ili uwe mfano mwema unaofuatwa katika kheri. Usikumbwe na uvivu wala udhaifu kama ilivyowapata wengi, bali vumilia, endelea kuwa na subira na muombe Mola wako msaada na tawfiyq. Aidha ni juu yako kutumia hekima, mtindo mzuri, subira na uvumilivu na kuchagua nyakati muafaka katika kuwakumbusha watu, kuwaalika kwenye kheri na kubainisha yale uliyoona katika jamii yako, nyumbani mwako, kabila lako au sehemu nyingineyo.
[1] 12:108
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2200/واجب-من-اقام-في-بيىة-فيها-منكرات-لم-تنكر
Imechapishwa: 19/07/2026
https://firqatunnajia.com/katika-hali-hii-inakupasa-kuamrisha-mema-na-kukemea-maovu/