Kanuni ni kwamba jambo lolote linalosemwa na baadhi ya wanazuoni au linalosemwa na wanazuoni wengi, kisha wengine wakalipinga, basi mwenye kutoa uamuzi juu yake ni Qur-aan cha Allaah na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.”[1]

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ

”Jambo lolote lile mlilokhitilafiana kwalo, basi hukumu yake ni kwa Allaah.”[2]

Hivyo basi yale ambayo watu wanakhitalifiana juu yake, basi hukumu yake inarejeshwa kwa Allaah na Mtume Wake. Yanarejeshwa katika Qur-aan na Sunnah. Linaloafikiana na Qur-aan na Sunnah au mojawapo kati ya viwili hivyo, basi hilo ndilo haki. Kinachoenda kinyume na viwili hivyo, basi kinarejeshwa kwa anayekisema hata kama anayekisema ni mtu mkubwa, mwenye cheo kikubwa au mwenye heshima kubwa. Kwa hakika Sunnah na haki ni vikubwa na bora zaidi kuliko mtu yeyote.

[1] 04:59

[2] 42:10

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2183/حكم-رفع-اليدين-بعد-الفريضة-للدعاء
  • Imechapishwa: 19/07/2026