Swali: Ni ipi hukumu iwapo mwanamke tajiri atamlipia mwanaume mahari yake?
Jibu: Hakuna tatizo. Iwapo mwanamke atamlipia mwanaume mahari yake, hakuna ubaya. Lakini ni lazima mwanaume ampe mwanamke kitu fulani, hata kama ni kidogo. Lazima ampe angalau kitu, kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم
”… mtafute [kuwaoa] kwa mali zenu… ”[1]
Kwa hiyo ikiwa mwanamke atampa mwanaume kitu cha kusaidia mahitaji, kama kununua fanicha ya nyumba au kumpa cha kuandaa karimu ya ndoa, Allaah amlipe kheri. Hili ni jambo jema. Katika baadhi ya nchi kama India, Pakistan na maeneo mengine mwanamke ndiye anayemlipia mwanaume. Iwapo mwanamke atamlipia mwanaume, basi hakuna tatizo. Lakini ni lazima mwanaume ampe mwanamke kitu fulani, hata kama ni kiasi kidogo mfano pesa kumi, mia au elfu. Lazima ampe kitu ili itimie maana ya kwamba amemchumbia kwa mali yake, kama ilivyokuja katika Aayah.
Kwa hiyo ni lazima kuwepo mahari kutoka kwa mwanaume, hata kama ni ndogo sana, ndipo ndoa ifungwe juu yake. Kilichobaki mwanamke atakitumia yeye mwenyewe na yeye atalipwa thawabu kwa hilo. Hakuna ubaya.
Kuna jambo jingine lililosahaulika kulitaja na hata baadhi ya Mashaykh hawakulitaja kwa ninavyokumbuka. Suala la kutafuta mchumba. Hakuna tatizo kwa mwanaume kumtafutia mchumba msichana au dada yake. Anaweza kumwambia mwanaume fulani kuwa anapenda kumuozesha msichana au dada yake. Kama vile mwanaume anavyomchumbia mwanamke, vivyo hivyo walii wa mwanamke anaweza kutafuta mchumba kwa ajili yake. Hili lilifanywa na baadhi ya Maswahabah. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alifanya hivyo na wengine pia walifanya. Kwa hiyo lengo ni kwamba mtu kumtafutia dada yake au binti yake mwanaume mwema, mwenye dini na uongofu na kumwambia kuwa yeye hana tamaa ya mali na kwamba atamuoza hata kwa mahari ndogo, kwamba yeye anaye msichana au dada yake anayependa amuoe na kwamba kama anapenda kumtazama basi ni vyema. Iwapo ataridhia basi akamuozesha kwa mahari ndogo. Hili linasaidia kuwepo kwa ndoa na kupunguza ugumu na gharama zisizo za lazima.
Mwanafunzi: Watu si watanidharau?
Ibn Baaz: Usiwajali. Ikiwa Allaah ameridhika nawe, basi watu hawana athari yoyote.
[1] 04:24
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2124/حكم-دفع-المراة-مهرها-لزوجها
- Imechapishwa: 19/07/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2124/حكم-دفع-المراة-مهرها-لزوجها
Imechapishwa: 19/07/2026
https://firqatunnajia.com/mwanamke-kumpa-mahari-mwanaume-amuoe/