Mwanamke ameswali miguu na mikono wazi

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuswali mikono na miguu wazi pamoja na kujua ya kwamba yuko nyumbani kwake na hayuko mbele ya wanaume?

Jibu: Maoni yanayotambulika ya Hanaabilah ni kwamba mwili wote wa mwanamke muungwana na ambaye kishabaleghe ni uchi wakati anapoliswa isipokuwa uso wake tu. Kujengea juu ya haya ni kwamba haifai kwake kufunua uso wala miguu yake. Wanazuoni wengine wengi wameonelea kufaa kwa mwanamke kuonyesha miguu na mikono yake. Kwa ajili hiyo salama zaidi ni mwanamke avifunike. Lakini ikiwa endapo itakadiriwa kuwa mwanamke ameswali miguu na mikono wazi kisha baadaye ndio akaja kuomba fatwa, basi inakuwa vigumu kwa mtu kumwamrisha kurudia kuswali.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/295)
  • Imechapishwa: 03/05/2026