Mwanamke aliye katika eda ya kufiliwa kutoka kwenda karamu ya harusi

Swali: Kuna mwanamke yumo ndani ya eda na amealikwa kuhudhuria karamu ya harusi na karamu nyenginezo. Je, ni wajibu kwake kuitikia myaliko hiyo? Ni dharurah zipi zinazomruhusu kutoka?

Jibu: Kuhusu usiku haijuzu kwake kuitikia wito. Kwa sababu si halali kwake kutoka usiku isipokuwa kwa kuwepo dharurah. Dharurah hizo ni kama nyumba kuchomeka, kuchelea inataka kuanguka, khofu ya wezi na mfano wa hayo.

Ama kuhusu mchana jambo ni pana. Akialikwa kwenye walima, ikiwa wale waliomwalika iwapo hatokuja basi hawatompa udhuru. Isitoshe pengine wakawa ni ndugu ambao ni lazima awaitikie mwaliko wao, hakuna neno akaenda katika mwaliko na akarudi pale tu karamu itapowisha. Vinginevyo bora kwake ni kubaki nyumbani katika hali zote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1291
  • Imechapishwa: 14/10/2019