Swali: Je, inajuzu kwa mwanafunzi kuingia katika chuo cha sheria ambacho anajifunza ndani yake sheria za kutungwa na baada ya hapo anamtetea dhalimu na aliyedhulumiwa na pia anaacha Shari´ah?
Jibu: Hakuna ubaya katika hilo. Lakini aanze na Shari´ah na azingatie Shari´ah. Ikiwa atasoma katika chuo cha sheria ili ajue mapungufu ya sheria za kibinadamu na njia za watu wake ili abainishe ubora wa haki juu yake na kwamba haki aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imeizidi na kuishinda na imeonyesha yale yenye maslahi ya jamii, basi hili ni jambo jema. Lakini asianze na hilo. Badlaa yake aanze na kile chenye manufaa zaidi. Aanze na chuo cha Shari´ah katika misingi ya dini, ajifunze dini yake na apate ufahamu katika hilo. Ikiwa kuna haja ya kuingia katika chuo cha sheria ili ajue mapungufu ya mifumo batili na ajue namna ya kuyajibu, basi hapana vibaya katika hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3502/حكم-دراسة-القوانين-الوضعية-لبيان-عوارها
- Imechapishwa: 04/09/2026
Swali: Je, inajuzu kwa mwanafunzi kuingia katika chuo cha sheria ambacho anajifunza ndani yake sheria za kutungwa na baada ya hapo anamtetea dhalimu na aliyedhulumiwa na pia anaacha Shari´ah?
Jibu: Hakuna ubaya katika hilo. Lakini aanze na Shari´ah na azingatie Shari´ah. Ikiwa atasoma katika chuo cha sheria ili ajue mapungufu ya sheria za kibinadamu na njia za watu wake ili abainishe ubora wa haki juu yake na kwamba haki aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imeizidi na kuishinda na imeonyesha yale yenye maslahi ya jamii, basi hili ni jambo jema. Lakini asianze na hilo. Badlaa yake aanze na kile chenye manufaa zaidi. Aanze na chuo cha Shari´ah katika misingi ya dini, ajifunze dini yake na apate ufahamu katika hilo. Ikiwa kuna haja ya kuingia katika chuo cha sheria ili ajue mapungufu ya mifumo batili na ajue namna ya kuyajibu, basi hapana vibaya katika hilo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3502/حكم-دراسة-القوانين-الوضعية-لبيان-عوارها
Imechapishwa: 04/09/2026
https://firqatunnajia.com/mwanafunzi-kusomea-kazi-ya-uanasheria/