Swali: Dada yangu anasoma kwa mmoja katika waalimu wa kike ambaye mara nyingi anamtukana Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah), anasema kuwa amekosea na mengine mengi. Je, dada yangu aendelee kusoma kwake?

Jibu: Hapana, hapana. Usisome kwa ambaye anamtukana mmoja katika maimamu wa Ahl-us-Sunnah, kama vile Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah). Ataathirika naye na kumuigiliza. Kwa hiyo haijuzu kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 16/11/2023