Swali: Vipi kuhusu kuwekwa Motoni milele muuaji muumini?
Jibu: Kuna umilele wa aina mbili inapokuja kwa muuaji na wengineo:
1 – Kuishi milele kwa daima. Aina hii ni kwa makafiri.
2 – Kuishi milele kwa muda fulani. Hili ndio lililokusudiwa kwa ambaye ni muuaji na mzinzi:
يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا
”Ataongezewa adhabu maradufu siku ya Qiyaamah na atadumu humo hali ya kutwezwa.”[1]
Hili ni kwa mzinzi na muuaji. Vilevile kisa cha yule bwana aliyejiua ambaye imepokelewa kwamba atawekwa Motoni milele. Kwa hivyo ni kuwekwa milele kwa muda fulani ambako kuna mwisho, tofauti na umilele wa makafiri ambao hauna mwisho. Waarabu wanajua hili. Hutumia neno “kudumu milele” kwa kitu cha muda mrefu. Wanasema:
“Walikaa ambapo wakadumu.”
Wakikusudia kwamba walikaa kwa muda mrefu.
[1] 25:69
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25078/هل-قاتل-المومن-يخلد-في-النار
- Imechapishwa: 31/01/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)