Thawabu kwa aliyepatwa na msiba na asisubiri?

Swali: Je, mtu analipwa thawabu akipatwa na msiba na asisubiri?

Jibu: Ikiwa atakata tamaa, hapana. Kinyume chake ni mwenye kupewa matishio:

”… na mwenye kuchukizwa, basi anapata hasira.”

Lakini hilo halizuii kuwa msiba huo unaweza kufuta madhambi hata kama hakusubiri. Hata hivyo hatopata ujira ambao Allaah huwapa wenye kusubiri. Lakini msiba kama msiba ni wenye kufuta madhambi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25077/هل-يوجر-من-اصيب-بمصيبة-ولم-يصبر
  • Imechapishwa: 31/01/2025