Mtenda madhambi amefuata matamanio yake?

Swali: Je, mwenye kuendelea juu ya madhambi anaingia ndani ya maneno Yake (Ta´ala):

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ تَذَكَّرُونَ

“Je, umemuona yule aliyejifanyia matamanio yake kuwa ndio mungu wake.”[1]

Jibu: Kwa upande wa kufata matamanio, na si kwamba huyu anayefuata matamanio yake anakuwa kafiri. Ni mtenda madhambi. Hivyo mzinifu na mwizi wamefuata matamanio yao, msengenyi na mbea wamefuata matamanio yao. Lakini kufuata matamanio ni kupeana zaidi kuliko shirki. Kila mshirikina amefuata matamanio yake, lakini si kila mwenye kufuata matamanio yake ni mshirikina ambaye amefanya shirkii kubwa. Na nani anayesalimika na kufuata matamanio kwa ujumla?

[1] 45:23

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25072/هل-يدخل-المصر-على-المعصية-فيمن-اتخذ-الهه-هواه
  • Imechapishwa: 31/01/2025