Swali: Ikiwa mwanamke katika zama zetu anafanya kazi ya ualimu na muda wake mwingi uko nje ya nyumba – Je, matumizi yanawajibika juu ya mume kwake? Afanye nini na mshahara wake?
Jibu: Hili hutofautiana. Ikiwa aliingia katika ndoa kwa sharti baina yake na mume wake kwamba anaruhusiwa kufundisha na mshahara wake ni wake, basi mume anawajibika kutekeleza wajibu wake wa matumizi juu yake, kwani yeye ni mke wake. Aidha aliingia katika hilo kwa ujuzi na kwa sharti na waislamu wapo juu ya masharti yao. Naye mwanamke ni juu yake kutekeleza wajibu wake anaporudi kutoka kazini, atekeleze wajibu wa nyumba na wajibu wa mume na mume atekeleze wajibu wake. Wote wawili washirikiane juu ya kheri na kumcha Allaah.
Ama wakizozana basi mahakama itawatenganishia. Wakikubaliana kwamba atampa nusu ya mshahara, mshahara wote au robo ya mshahara kwa sababu ya yeye kumruhusu kufanya kazi, basi hili ni jambo baina yao. Wakikubaliana juu ya jambo fulani, basi hakuna tatizo baina yao. Wakizozana, basi mahakama itahukumu baina yao, au baadhi ya majirani au baadhi ya jamaa zao waingilie kati na wasuluhishe baina yao ili wasifike kwenye mahakama.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2174/حكم-انفاق-الزوج-على-امراته-الموظفة
- Imechapishwa: 10/07/2026
Swali: Ikiwa mwanamke katika zama zetu anafanya kazi ya ualimu na muda wake mwingi uko nje ya nyumba – Je, matumizi yanawajibika juu ya mume kwake? Afanye nini na mshahara wake?
Jibu: Hili hutofautiana. Ikiwa aliingia katika ndoa kwa sharti baina yake na mume wake kwamba anaruhusiwa kufundisha na mshahara wake ni wake, basi mume anawajibika kutekeleza wajibu wake wa matumizi juu yake, kwani yeye ni mke wake. Aidha aliingia katika hilo kwa ujuzi na kwa sharti na waislamu wapo juu ya masharti yao. Naye mwanamke ni juu yake kutekeleza wajibu wake anaporudi kutoka kazini, atekeleze wajibu wa nyumba na wajibu wa mume na mume atekeleze wajibu wake. Wote wawili washirikiane juu ya kheri na kumcha Allaah.
Ama wakizozana basi mahakama itawatenganishia. Wakikubaliana kwamba atampa nusu ya mshahara, mshahara wote au robo ya mshahara kwa sababu ya yeye kumruhusu kufanya kazi, basi hili ni jambo baina yao. Wakikubaliana juu ya jambo fulani, basi hakuna tatizo baina yao. Wakizozana, basi mahakama itahukumu baina yao, au baadhi ya majirani au baadhi ya jamaa zao waingilie kati na wasuluhishe baina yao ili wasifike kwenye mahakama.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2174/حكم-انفاق-الزوج-على-امراته-الموظفة
Imechapishwa: 10/07/2026
https://firqatunnajia.com/mume-kumhudumia-mke-wake-mwajiriwa/