Wanaolipwa mishahara katika idara mbalimbali bila ya kufanya kazi

Swali: Mimi ni mwajiriwa katika idara ya serikali. Idara hii huwateua wafanyakazi wake kufanya kazi nje ya muda wa kazi, jioni ya alkhamisi na siku ya ijumaa. Hakuna yeyote miongoni mwa walioteuliwa anayekuja kufanya kazi. Baada ya Allaah kuniongoza katika haki nilimuomba meneja wa masuala ya wafanyakazi awasimamie wafanyakazi katika kazi na asiwateue. Lakini hakusikiliza maneno yangu, kwa sababu naye huteua pamoja nasi na hahudhurii. Pia niliomba jina langu liondolewe katika uteuzi huo hali ya kuwa ninahitaji kiasi hiki cha pesa, kwa sababu ninahudumia familia kubwa. Kiasi hiki cha pesa ikiwa sitokichukua mimi, basi kitachukuliwa na mwingine kwa njia yoyote ile. Ni lipi suluhisho?

Jibu: Hili halijuzu. Huu ni ukhaini kutoka kwa anayeamrisha na wanaoamrishwa wote. Kuamrisha bila kazi, huu ni ukhaini. Watu wanapofanya ukhaini, usifanye ukhaini pamoja nao. Watu wanapofanya ukhaini, usifanye ukhaini pamoja nao. Hata kama wao wamefanya ukhaini, hata kama wamechukua mali. Hukumu inawahusu wote watatu. Usiwe pamoja na wafanyao ukhaini.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2224/الانكار-على-من-يتعاطى-اجرا-بدون-عمل
  • Imechapishwa: 10/07/2026

Turn on/off menu