Swali: Kuna mtu amekusanya mali kwa njia isiyokubalika katika Shari´ah kisha akatubu. Ni ipi hukumu ya mali iliyoko mikononi mwake?
Jibu: Ni juu yake atubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na arudishe mali kwa wenyewe. Ikiwa aliichukua kwa njia isiyokubalika katika Shari´ah, basi airudishe kwa wenyewe. Ikiwa aliinyang´anya mtu au aliiba kutoka kwa mtu. Ikiwa ilitokana na muamala mbovu, basi amche Allaah na atoe swadaqah kile kilichozidi juu ya halali. Kile anachokijua hali ya kuwa ni halali akibakize, na kile anachokijua hali ya kuwa ni haramu akitumie katika njia za kheri, kama kuwapa maskini, kujenga au kurekebisha vyoo vya misikiti na mfano wa hayo. Wala asile kitu anachokijua ni haramu. Allaah anakubali tawbah yake. Kwa maana ajitahidi kubakiza halali na kile kilichozidi juu ya halali ambacho anajua ni batili na kimeingia kwake kwa njia isiyo ya Kishari´ah. Ikiwa wamiliki wanajulikana, basi airudishe kwao. Ikiwa hawajulikani au anaogopa khatari katika kuirudisha, basi atoe swadaqah katika njia za kheri na matendo mema.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2179/حكم-من-جمع-مالا-بطريقة-غير-شرعية-ثم-تاب
- Imechapishwa: 10/07/2026
Swali: Kuna mtu amekusanya mali kwa njia isiyokubalika katika Shari´ah kisha akatubu. Ni ipi hukumu ya mali iliyoko mikononi mwake?
Jibu: Ni juu yake atubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na arudishe mali kwa wenyewe. Ikiwa aliichukua kwa njia isiyokubalika katika Shari´ah, basi airudishe kwa wenyewe. Ikiwa aliinyang´anya mtu au aliiba kutoka kwa mtu. Ikiwa ilitokana na muamala mbovu, basi amche Allaah na atoe swadaqah kile kilichozidi juu ya halali. Kile anachokijua hali ya kuwa ni halali akibakize, na kile anachokijua hali ya kuwa ni haramu akitumie katika njia za kheri, kama kuwapa maskini, kujenga au kurekebisha vyoo vya misikiti na mfano wa hayo. Wala asile kitu anachokijua ni haramu. Allaah anakubali tawbah yake. Kwa maana ajitahidi kubakiza halali na kile kilichozidi juu ya halali ambacho anajua ni batili na kimeingia kwake kwa njia isiyo ya Kishari´ah. Ikiwa wamiliki wanajulikana, basi airudishe kwao. Ikiwa hawajulikani au anaogopa khatari katika kuirudisha, basi atoe swadaqah katika njia za kheri na matendo mema.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2179/حكم-من-جمع-مالا-بطريقة-غير-شرعية-ثم-تاب
Imechapishwa: 10/07/2026
https://firqatunnajia.com/kujikwamua-na-mali-ya-haramu-ii/