Swali: Je, inajuzu kuchomoa kabla ya kumwaga ndani kwa lengo la kumlea mtoto katika hali ya kunyonyeshwa kwa maziwa ya kopo kutokana na ugonjwa ulioko katika titi la mama yake?
Jibu: Asili ya jambo hilo ni kwamba inajuzu, huo ndio msingi. Inajuzu kuchomoa kabla ya kumwaga ndani kwa maslahi yanayokubalika katika Shari´ah na kwa sababu ambazo wanandoa wanakubaliana juu yake. Lakini inatakiwa isiwe ya muda mrefu, kwa sababu jambo hilo mara nyingi linaweza kusababisha matatizo kwa wote. Lakini ikiwa ni katika muda mfupi, kama ilivyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo Jaabir amesema:
”Tulikuwa tukifanya al-´Azl na huku Qur-aan ikishuka.”
Kama ingekuwa ni jambo lililokatazwa basi Qur-aan ingetukataza. Kwa hiyo kuchomoa kabla ya kumwaga ndani ni jambo lilikuwepo katika zama zake na hakulikataza.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2191/هل-يجوز-العزل-بغرض-تربية-الطفل
- Imechapishwa: 10/07/2026
Swali: Je, inajuzu kuchomoa kabla ya kumwaga ndani kwa lengo la kumlea mtoto katika hali ya kunyonyeshwa kwa maziwa ya kopo kutokana na ugonjwa ulioko katika titi la mama yake?
Jibu: Asili ya jambo hilo ni kwamba inajuzu, huo ndio msingi. Inajuzu kuchomoa kabla ya kumwaga ndani kwa maslahi yanayokubalika katika Shari´ah na kwa sababu ambazo wanandoa wanakubaliana juu yake. Lakini inatakiwa isiwe ya muda mrefu, kwa sababu jambo hilo mara nyingi linaweza kusababisha matatizo kwa wote. Lakini ikiwa ni katika muda mfupi, kama ilivyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo Jaabir amesema:
”Tulikuwa tukifanya al-´Azl na huku Qur-aan ikishuka.”
Kama ingekuwa ni jambo lililokatazwa basi Qur-aan ingetukataza. Kwa hiyo kuchomoa kabla ya kumwaga ndani ni jambo lilikuwepo katika zama zake na hakulikataza.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2191/هل-يجوز-العزل-بغرض-تربية-الطفل
Imechapishwa: 10/07/2026
https://firqatunnajia.com/uzazi-wa-mpango-ili-mtoto-apate-kukuwa/