Mume kuangalia uchi wa mke wake

Swali: Inajuzu kwa mwanaume kuangalia uchi wa mke wake na ni upi mpaka ulioruhusiwa?

Jibu: Ni sawa. Kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hifadhi ´Awrah yako isipokuwa kwa mke wako na wale iliyomiliki mikono yako ya kiume.”

Mtu akitaka kutazama uchi wa mke wake inajuzu kwake kutazama. Hili ni suala maalum baina ya wanandoa. Hukumu iko wazi:

“Hifadhi ´Awrah yako isipokuwa kwa mke wako na wale iliyomiliki mikono yako ya kiume.”

Ameamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhifadhi ´Awrah isipokuwa yale ambayo Shari´ah imeyavua; mke wako na wale iliyomiliki mikono yako ya kiume.

Swali: Kuna mtu anauliza swali na sauti haisikiziki…

Jibu: Hadiyth hii sio sahihi. Hadiyth isemayo:

“Sikuona kutoka kwake na wala yeye hakuona kutoka kwangu.”

Sio sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.njza.net/Default_ar.aspx?ID=98
  • Imechapishwa: 22/09/2020