Swali: Kuna mwanaume alimuomba mke wake yale ambayo mume humuomba mke wake na ilikuwa mchana wa siku ya Alkhamisi. Akasema [mke] mimi nimeamka na swawm ilihali yeye [mume] hakuwa ni mwenye kujua hilo. Kisha mke akasema “Haina neno ikiwa jambo hili waliridhia”. Je, kuna kitu chochote juu ya hili?

Jibu: Ikiwa swawm ni ya faradhi, mume hatakiwi kumuomba. Kwa mfano analipa swawm ya Ramadhaan, kafara n.k., hatakiwi kumtaka kujamiiana naye akamuharibishia swawm yake. Ama ikiwa ni sunnah, hakuna neno. Akitaka kula, anaweza kula na isitoshe hatakiwi kufunga pasina idhini ya mume wake. Ikiwa mume wake yupo, hatakiwi kufunga pasina idhini yake. Kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Asifunge mwanamke na mume wake yupo [hakusafiri] isipokuwa kwa idhini yake.”

Isipokuwa Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12824
  • Imechapishwa: 21/11/2014