Swali: Mara nyingi tunasikia kukisemwa “´Aqiydat-us-Salaf”. Tunataraji kutoka kwako utubainishie ni ipi Manhaj ya Salaf na Salafiyyah?

Jibu: ´Aqiydah ya Salaf ni kumpwekesha Allaah na kumtii na kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yaliyotolewa dalili na Qur-aan. Hii ndio ´Aqiydah ya Salaf. Kumpwekesha na kumtakasia ´ibaadah Allaah na kumtekelezea aina zote za ´ibaadah Allaah na kutahadharisha kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla). Kumuamini Allaah, siku ya Mwisho, Malaika, Vitabu, Mitume na Qadar; kheri na shari yake. Kuamini Majina na Sifa za Allaah na kumthibitishia nazo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kwamba yuko juu ya ´Arshi, juu ya viumbe vyote, Amelingana juu ya ´Arshi, kuwa juu ambako kulingana na Utukufu na Ukubwa Wake, na kwamba Yeye ni al-´Aliyy [Yuko juu] ya viumbe vyote:

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake Pekee linapanda neno zuri na kitendo chema Hukipa hadhi.” (35:10)

وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

”Naye ni Al-‘Aliyyul-‘Adhwiym (Mwenye Uluwa – Mwenye taadhima).” (02:255)

Kuamini ya kwamba Ujuzi Wake umeenea kila mahali. Hii ndiyo ´Aqiydah ya Salaf. Pamoja na kuamini ya kwamba Imani inazidi na kupungua. Maasi yanayapunguza Imani na kuidhoofisha, lakini hata hivyo haitoweki Imani (moja kwa moja), tofauti na wanavyoamini Khawaarij na Mu´tazilah. Imani inazidi na kupungua, tofauti na Khawaarij na Mu´tazilah.

Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni pamoja na kuamini ya kwamba Imani inazidi na kupungua na kwamba wafanya madhambi; mzinifu na mwenye kuiba, Imani zao hazitoweki maadamu hajahalalisha hilo. Imani zao zinapungua. Akifa juu ya Zinaa, kuiba, kuwaasi wazazi wawili, juu yake ana matishio ya Allaah. Anakhofiwa juu yake Moto isipokuwa ikiwa kama Allaah Atamsamehe. Lakini hata hivyo Imani yake haitoweki (moja kwa moja) kwa kufanya hayo, tofauti na Khawaarij na Mu´tazilah. Kutokana na Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa; lakini Anasamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.” (04:48)

Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Kumuamini Allaah, Majina Yake, Sifa Zake na kwamba vinalingana na Utukufu na Ukubwa unaolingana na Allaah, Yuko juu ya ´Arshi, juu ya viumbe Vyote na Elimu (Ujuzi) Wake uko kila mahali na hafichikani na kitu chenye kujificha na kwamba Imani inazidi na kupungua. Inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi. Hii ndio kauli ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah tofauti na Khawaarij na Mu´tazilah ambao wanasema kuwa haizidi na wala haipungui. Vilevile tofauti na Mur-jiah ambao wanayatoa matendo katika Imani. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wao wanasema:

“Imani ni kauli na ´amali na kuamini. Inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi.”

Imani hayaivunji [kwa maasi chini Shirki], isipokuwa kitu kinachoivunja Imani ni kufuru. Kukipatikana kwake kitu katika kumkufuru Allaah au Shirki, inavunjika. Ama maasi, kuwaasi wazazi wake wawili au mmoja wao, akazini lakini akawa hakuhalalisha hilo, akaiba, akanywa pombe na kadhalika, haya yote yanayapunguza Imani na inakuwa dhaifu. Hawi kafiri. Hata hivyo ameahidiwa kupata adhabu na yuko katika khatari kubwa. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hazini mwenye kuzini pale anapozini ilihali ni muumini. Hanywi mwenye kunywa pombe pale anapokunywa ilihali ni muumini. Haibi mwenye kuiba pale anapoiba ilihali ni muumini.”

Maana yake ni kwamba hawi muumini kwa kuwa na Imani kamilifu. Kilichompeleka kufanya maasi haya ni kutokana na upungufu na udhaifu wa Imani yake. Kwa ajili hii ndio maana akizini anasimamishiwa hadd (adhabu) na wala hakufuru. Akinywa pombe anasimamishiwa hadd na wala hakufuru maadamu hajahalalisha hayo. Hii ndio kauli ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, tofauti na Khawaarij, Mu´tazilah na Murji-ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12824
  • Imechapishwa: 20/11/2014