Mume anataka anunuliwe gari na mke

Swali: Mume wangu ananiomba nimnunulie gari. Mimi ni mfanya kazi na mshahara wangu nautumia mimi mwenyewe na watoto wangu. Je, inajuzu kwake [mume] kufanya hivo?

Jibu: Kinyume chake. Wajibu ni juu yake yeye kumhudumia mke wake hata kama atakuwa ni tajiri. Matumizi ya mke yako juu ya mume hata kama atakuwa ni tajiri.

Lakini akimkirimu mume wake na akamsaidia au akamnunulia gari, huku ni katika kuishi vizuri na ni jambo zuri. Ama mume kushurutisha hilo, hapana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo_%20maftuh-20-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/05/2015