Swali: Baadhi ya wanafunzi, au angalau kwa uchache watu wanaojinasibisha na kusoma, wanasema kuwa wale waliolipua Saudi Arabia walifanya Ijtihaad na wakakosea na kwamba ni jambo la kupitiliza kuwakemea kwa ukali. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Ina maana kwamba ni wenye kupatia na wanalipwa thawabu. Walifanya Ijtihaad ingawa hawakupatia ina maana ya kwamba wana thawabu. Ni maneno batili. Nyumba za Allaah zinatakiwa kulindwa na mambo kama hayo. Hivi kweli mtu mwenye kulipua waswalaji katika Rukuu´ au Sujuud apewe udhuru kwa sababu ni Mujtahid? Ni Mujtahid? Namna gani amekuwa Mujtahid?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Waswiyyat-un-Nabiy http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/wasiyah%20nabi-21-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 08/07/2018