Muislamu kuanza kumsalimia kafiri

Swali: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametukataza kuanza kuwatolea makafiri Salaam. Je, makatazo haya yanaishia kuwaambia “as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah” au ni makatazo ambayo kunaingia ndani yake mamkizi aina yote? Je, inajuzu kuanza kumsalimia jirani ambaye ni mnaswara kinyume na kusema “as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah” kama kumwambia “Khabari yako”, “Vipi hali yako” au “Khabari ya asubuhi”?

Jibu: Haijuzu kuanza kumtolea kafiri Salaam kutokana na yaliyothibiti kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msianze kuwatolea mayahudi na manaswara Salaam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbane kandoni.”

Ameipokea Muslim.

Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahl-ul-Kitaab wakikusalimieni waambieni “wa ´alaykum.”

Wanatakiwa kuitikiwa kutokana na udhahiri wa Hadiyth kwa kuambiwa:

“wa ´alaykum.”

Hata hivyo hakuna ubaya kumsalimia kafiri kwa kumwambia:

“Vipi hali yako”, “Umeamkaje”, “Umelalaje” na mfano wa maamkizi kama hayo kukiwa kuna haja ya kufanya hivo. Hivyo ndivyo wanavyoonelea baadhi ya wanachuoni ikiwa ni pamoja na Abul-´Abbaas Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/312)
  • Imechapishwa: 23/08/2020