Mtoto wa nje ya ndoa ataingia Peponi?

Swali: Je, mtoto wa zinaa ataingia Peponi? Imesemekana kuwa mtoto wa zinaa ni najisi na Peponi hakuingii mnajisi.

Jibu: Akifa hali ya kuwa ni muislamu ataingia Peponi. Kuwa kwake mtoto wa nje ya ndoa sio kikwazo. Mtoto wa nje ya ndoa sio najisi. Dhambi ya uzinzi ni kwa yule mzinifu na sio kwa yule aliyeumbwa kwa manii ya zinaa. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ

“Na wala mbebaji [wa dhambi] hatabeba mzigo wa mwengine.” (17:15)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muislamu hanajisiki.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/350-351)
  • Imechapishwa: 23/08/2020