Kuwaombea msamaha mababu waliokufa katika shirki

Swali: Mimi nina mababu waliokufa juu ya shirki. Je, naweza kuwaombea msamaha au hapana?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kuwaombea msamaha mababu zake wala watu wengine ikiwa wamekufa juu ya shirki. Amesema (Ta´ala):

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ

“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni.” (09:113)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/305)
  • Imechapishwa: 23/08/2020