Swali: Kuna mtu alikuwa ni muislamu kisha akaritadi kutoka katika Uislamu na akafa katika hilo. Je, tunaweza kusema kuwa ni kafiri? Ni ipi hukumu kwa mwenye kuritadi kutoka katika Uislamu? Je, tunaweza kumuombea msamaha kwa Allaah kama kusema “Allaah msamehe dhambi zake?”

Jibu: Ambaye alikuwa muislamu kisha akaritadi ni kafiri. Anatakiwa kuambiwa atubu kwa siku tatu, akitubu ni sawa, la sivyo auawe. Haijuzu kumuombea msamaha akifa katika kuritadi. Amesema (Ta´ala):

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ

“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni.” (09:113)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/304)
  • Imechapishwa: 23/08/2020