Muhrim anasema nini wakati anapopita kwenye jiwe jeusi?

Swali: Nini anachosema Muhrim wakati anapopita jiwe jeusi?

Jibu: Aashirie kwa mkono wake na kusema:

الله أكبر

“Allaah ni mkubwa.”

Halafu aendelee Twawaaf yake. Hivyo anafanya pale ambapo hawezi kufika kwenye jiwe. Ama ikiwa anaweza kufika kwenye jiwe aliguse kwa mkono wake na alibusu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqu-%2020-08-1435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015