Swali: Tunapenda useme kitu kuhusiana na mbadiliko wa uvaaji kwa wanawake katika nchi hii. Kwa sasa anaweka ´Abaa´ah yake mabegani na Niqaab na sehemu ya uso wake inaonekana.

Jibu: ´Abaa´ah haiwekwi mabegani kwa mwanamke wakati anapotoka. Wakati anapotoka aweke ´Abaa´ah yake kichwani. Isitiri kichwa chake, mavazi na mabega yake. Ni lazima aweke ´Abaa´ah kichwani wakati anapotoka nje.

Ama kuhusiana na Hijaab [mtandio], afunike kichwa chake ili kusionekane kitu isipokuwa macho tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqu-%2020-08-1435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015