Msafiri anaswali ´Ishaa kabla ya wakati wake

Swali: Mimi kama msafiri nina haki ya kuswali ´Ishaa kabla ya wakati wake nikisahau kujumuisha baina ya Maghrib na ´Ishaa?

Jibu: Hapana. Usiiswali kabla ya wakati wake ikiwa kama hukuijumuisha na ile swalah ya kwanza. Kwa kuwa ukiijumuisha na ile swalah ya kwanza wakati wake unakuwa mmoja. Ikiswa hazikujumuishwa kila swalah itaswali katika wakati wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqu-%2020-08-1435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015