Swali: Je, inafaa kwa mwenye janaba kusikiliza Qur-aan iliyorekodiwa?

Jibu: Hapana neno kwa hilo. Ni mamoja imerekodiwa kwenye kanda, msomaji n.k. Muhimu yeye asisome Qur-aan. Ama kusikiliza hapana kizuizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (35)
  • Imechapishwa: 28/09/2023