Anamtaliki mke kwa lengo la kumnyima mirathi

Swali: Mwanaume akimtaliki mwanamke katika maradhi ya maututi kwa lengo la kumnyima mirathi – je, mke atamrithi ingawa ameshatoka ndani ya eda?

Jibu: Hapana ikiwa ameshatoka ndani ya eda. Sio mke tena. Akishatoka ndani ya eda sio mke tena. Lakini muda wa kuwa yuko ndani ya eda anazingatiwa bado ni mke.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (35)
  • Imechapishwa: 28/09/2023