Muda wa kutumia vidonge vya kuzuia ujauzito

Swali: Ni muda gani unaokubalika katika Shari´ah juu ya kutumia vidonge vinavyozuia ujauzito?

Jibu: Msingi ni kutokufaa kwa mwanamke kutumia vidonge vinavyozuia mimba. Kuna madhara ndani yake. Isipokuwa akilazimika kufanya hivo au ikamtokea haja. Haja ni kama vile anadhurika kwa kuzaa watoto, kunamdhuru afya yake au hawezi kuwalea. Katika hali kama hii hapana vibaya akatumia vidonge vinavyozuia kwa muda wa mwaka mmoja au miwili. Kwa sharti visiwe ni vyenye kumdhuru afya yake, visipelekee kukata kizazi na sharti nyingine awe mwenye kuhitajia jambo hilo au amelazimika.

Lakini akiwa si mwenye kuhitajia au vidonge hivi vinakatiza ujauzito au vinadhuru afya yake, basi haitofaa kwake kuvitumia. Vinatumiwa wakati wa dharurah au haja kubwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 05/11/2021