Amezidisha Rak´ah moja ya Witr ili aamke usiku kuswali tena

Swali: Baadhi ya watu wanaposwali Witr pamoja na imamu na imamu akatoa Tasliym husimama na wakaswali Rak´ah nyingine moja ili aswali Witr yake mwishoni mwa usiku. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi? Je, anazingatiwa amemaliza sambamba na imamu?

Jibu: Hatujui ubaya wowote juu ya hilo. Limetajwa na wanazuoni na halina neno. Ni ili aweze kuswali Witr yake mwishoni mwa usiku. Anaaminika kwamba amesimama pamoja na imamu mpaka akamaliza naye. Kwa sababu ameswali pamoja naye mpaka imamu akamaliza na akazidisha Rak´ah moja kutokana na manufaa yanayokubalika katika Shari´ah ili aswali Witr yake mwishoni mwa usiku. Hivyo hakuna neno kufanya hivo. Haimtoi nje kwamba hakusimama pamoja na imamu. Bali amesimama pamoja na imamu mpaka akamaliza naye. Lakini hakumaliza sambamba naye bali yeye amechelewa kidogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/312)
  • Imechapishwa: 05/11/2021