Swali: Muadhini akisema wakati wa kuadhini:
أشهدُ أنَّ محمَّدًا عبد الله ورَسولُه
”Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja wa Allaah na Mtume Wake.”
badala ya:
أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ الله
”Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah.”
Je, analazimika kuirudia sentesi hii?
Jibu: Ndio. Adhaana haibadilishwi, haizidishwi na wala haipunguzwi. Inatakiwa kusomwa kama ilivyopokelewa.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
- Imechapishwa: 19/05/2023