Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
عن أبي فِراسٍ ربيعةَ بنِ كعبٍ الأسلميِّ خادِمِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، ومن أهلِ الصُّفَّةِ رضي الله عنه، قَالَ: كُنْتُ أبِيتُ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم فآتِيهِ بِوَضُوئِهِ وَحَاجَتِهِ، فَقَالَ: (سَلْنِي) فقُلْتُ: اسْأَلُكَ مُرَافَقَتَكَ في الجَنَّةِ. فَقَالَ: (أَوَ غَيرَ ذلِكَ؟) قُلْتُ: هُوَ ذَاكَ، قَالَ: (فأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ بِكَثْرَةِ السُّجُودِ). رواه مسلم
106 – Abu Firaas, Rabiy´ bin Ka’b al-Aslamiy, mfanya kazi wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na pia ni katika watu wa Swuffah (Radhiya Allaahu ‘anh), amesimulia: “Nilikuwa nikilala kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) nikimpelekea maji ya kutawadhia na mahitaji yake mengineo. Akaniambia: “Niombe.” Nikasema: “Nakuomba kuwa pamoja nawe Peponi.” Akasema: “Hakuna jengine?” Nikasema: “Ni hilo tu.” Akasema: “Nisaidie juu nafsi yako kusujudu kwa wingi.” [1]
Ameipokea Muslim.
Katika Hadiyth hii tunapata faida juu ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hamiliki kumwingiza yeyote Peponi. Ndio maana hakumdhamini kumpa mtu huyu maombi yake. Hata hivyo badala yake amemwambia:
“Nisaidie juu nafsi yako kusujudu kwa wingi.”
Akisimama kwa kukithirisha sujudu nyingi ambazo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemuusia, hivyo anaweza kuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Peponi.
[1] Muslim (489).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/104-105)
- Imechapishwa: 16/01/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)