Swali: Yapi maoni yako kuweka mpaka siku maalumu kufanya khuruuj katika njia ya Allaah na Jamaa´t-ut-Tabliygh?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haikuthibiti kwake kwamba aliamrisha hilo kabisa. Na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa ni watu wenye hima kwa kheri na watu wenye kujikurubisha kwa yale Allaah Anayoyapenda. Haikupokelewa kutoka kwa mmoja katika yao (Radhiya Allaahu ´anhum) kitu katika hayo. Na ikiwa tutashindwa kufanya baadhi ya ´amali, tuko na mizani kamili; maneno ya Allaah na maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo basi, tukimbilie kujifunza Dini. Na mmoja wetu akitaka kubobea katika kitu, basi anaweza kuhifadhi na kufahamu maneno ya Mola wa viumbe na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hakika atakaeruzukiwa kufahamu Kitabu cha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na Sunnah za Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atakuwa ameruzukiwa kheri kubwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=130109&st=40
  • Imechapishwa: 03/09/2020