Swali: Yapi maoni yako kuweka mpaka siku maalumu kufanya khuruuj katika njia ya Allaah na Jamaa´t-ut-Tabliygh?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haikuthibiti kwake kwamba aliamrisha hilo kabisa. Na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa ni watu wenye hima kwa kheri na watu wenye kujikurubisha kwa yale Allaah Anayoyapenda. Haikupokelewa kutoka kwa mmoja katika yao (Radhiya Allaahu ´anhum) kitu katika hayo. Na ikiwa tutashindwa kufanya baadhi ya ´amali, tuko na mizani kamili; maneno ya Allaah na maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo basi, tukimbilie kujifunza Dini. Na mmoja wetu akitaka kubobea katika kitu, basi anaweza kuhifadhi na kufahamu maneno ya Mola wa viumbe na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hakika atakaeruzukiwa kufahamu Kitabu cha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na Sunnah za Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atakuwa ameruzukiwa kheri kubwa.
- Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=130109&st=40
- Imechapishwa: 03/09/2020
Swali: Yapi maoni yako kuweka mpaka siku maalumu kufanya khuruuj katika njia ya Allaah na Jamaa´t-ut-Tabliygh?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haikuthibiti kwake kwamba aliamrisha hilo kabisa. Na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa ni watu wenye hima kwa kheri na watu wenye kujikurubisha kwa yale Allaah Anayoyapenda. Haikupokelewa kutoka kwa mmoja katika yao (Radhiya Allaahu ´anhum) kitu katika hayo. Na ikiwa tutashindwa kufanya baadhi ya ´amali, tuko na mizani kamili; maneno ya Allaah na maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo basi, tukimbilie kujifunza Dini. Na mmoja wetu akitaka kubobea katika kitu, basi anaweza kuhifadhi na kufahamu maneno ya Mola wa viumbe na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hakika atakaeruzukiwa kufahamu Kitabu cha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na Sunnah za Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atakuwa ameruzukiwa kheri kubwa.
Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=130109&st=40
Imechapishwa: 03/09/2020
https://firqatunnajia.com/mtume-hakufanya-dawah-kwa-kutenga-siku-maalumu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)